Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

Vital Kamerhe aendelea kusalia jela

Vital Kamerhe mshirika wa karibu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado anazuiwa jela kwa madai ya ufisadi, baada ya mahakama kukataa kuachiliwa kwake licha ya shinikizo kutoka kwa chama chake cha UNC.

Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi.
Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuwa ikizua maoani mbalimbali kama alivyobaini Balozi Nicolas Kazadi ambaye alihusika na mpango wa mabadiliko ndani ya siku 100 katika serikali ya rais Tshisekedi.

Mashirika yasiyo ya kiserikali, lakini pia mashirika ya kiraia wanashutumu ofisi ya rais kutoa zabuni kwa upendeleo bila kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Baadhi ya mashirika kama vile ODEP au AMKA yanashuku kuwa pesa nyingi zilipitishwa mlango wa nyuma. Ikiwa Vital Kamerhe anakabikliwa na mashitaka hayo, ni kwa sababu yeye sio tu "afisa anayesimamia masuala ya gharama katika opfisi ya rais, lakini pia, kwa sababu hadi Septemba 2019, alikuwa anasimamia kwa mkono wa chuma fedha za mpango huo ”, vyanzo kutoka ofisi ya mashtaka, na vile kutoka kambi ya mshirika wake, Félix Tshisekedi vimebaini.

Watu kadhaa walikamatwa mwezi Machi mwaka jana kufuatia madai hayo, huku viongozi wa makampuni ya kibinafsi na yale ya umma wakiwekwa korokoroni kabla ya kuachiliwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.