Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Shambulio Somalia: Idara ya ujasusi yashutumu nchi ya kigeni

Nchini Somalia kumezuka sintofahamu baada ya shambulio baya kutokea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu, Jumamosi iliyopita, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu wengi.

Maafisa wa idara ya uokoaji wakibeba mwili wa mtu aliyeuawa katika shambulio la bomu Mogadishu, Somalia, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu wengi, Jumamosi, Desemba 28, 2019.
Maafisa wa idara ya uokoaji wakibeba mwili wa mtu aliyeuawa katika shambulio la bomu Mogadishu, Somalia, shambulio ambalo liligharimu maisha ya watu wengi, Jumamosi, Desemba 28, 2019. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii idara ya ujasusi ya Somalia iliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba nchi ymoja ya kigeni ilipanga shambulio hilo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. Lakini, kwa vile bomu lilikuwa limelenga msafara wa magari ya Uturuki, wengi walifikiria kwamba Falme za Kiarabu, ambazo zinapingana na Ankara katika ukanda huo ndio zilihusika na shambulio hilo.

Ujumbe huo wa idara ya ujasusi ya Somalia umezua zintofahamu katika ukanda huo.

Katika ujumbe wake, idara ya ujasusi (NISA) haikutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake hayo.

Ujumbe huo pia umewaacha vinywa wazi baadhi ya wanasiasa, hususan wale wa upinzani nchini Somalia.

Mbunge wa chama cha Wadajir, Abdirahman Abdishakur, amefutilia mbali "madai hayo ya yanapotosha umma ambayo lengo lake ni kujitetea kwa idara ya ujasusi baada ya kushindwa kutekeleza jukumu lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.