Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA-UGAIDI

Uturuki yatuma ndege ye kijeshi baada ya shambulizi nchini Somalia

Ndege ya kivita kutoka nchini Uturuki, iliwasili mjini Mogadishu nchini Somalia kuwasafirisha nje ya nchi watu waliojeruhiwa vibaya baada kutokea kwa shambulizi la bomu siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya watu 79.

Picha ya baada ya shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia
Picha ya baada ya shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Mbali na hilo ndege hiyo iliwasafirisha Madaktari kuja kuwatibu watu 125 waliojeruhiwa baada ya shambulizi hilo ambalo lilitokea baada ya gari lenye vilipuzi kulipuka.

Hakuna kundi lolote lililojitokeza kudai kutekeleza shambulizi hilo lakini rais Mohamed Abdullahi Farmaajo amelishtumu kundi la Al Shbab ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi kama haya.

Shambulizi la Jumamosi, lilikuwa baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo tangu mwaka 2017.

Kati ya watu 16  waliofariki walikuwa wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Binafsi Banadir kilichopo mjini Mogadishu waliokuwa safarini mara mlipuko ulipotokea kusini magharibi mwa jiji hilo.

Majeruhi wengi walibebwa kwa machela na kuondolewa katika eneo la mkasa ambapo mlipuko ulivuruga na kusalia mabaki ya magari.

Raia 2 wa Uturuki ni miongoni mwa waliouawa,kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya Uturuki ambayo iliarifu kupitia ukurasa wake wa Twita.

Bado haijajulikana nani hasa wahusika wa shambulizi hilo licha ya mashambulizi kadhaa kutekelezwa na kundi la kiislamu Al shabab ambalo limekuwa likipambana na serikali inayoungwa mkono na umoja wa mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.