Pata taarifa kuu
DRC-KINSHASA-BENI-MWAKA-MPYA-2020

DRC: Wakaazi wa Beni na Kinshasa waupokea mwaka mpya wa 2020 kwa bashasha

Wakaazi wa mji wa Beni, walijitokeza kwa wingi makanisani kuukaribisha mwaka mpya wa 2020, licha ya wasiwasi wa usalama katika eneo la Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Sehemu ya jiji la Kinshasa nchini DRC
Sehemu ya jiji la Kinshasa nchini DRC AFP PHOTO / PAPY MULONG
Matangazo ya kibiashara

Maelfu walikusanyika katika makanisa mbalimbali, wakiombea amani eneo hilo ambalo limeshuhudia mauaji makubwa ya raia mwaka 2019 ambapo kati ya mwezi Oktoba na Desemba, zaidi ya watu 200 walipoteza maisha.

Ulikuwa ni usiku wa shamrashamra katika maeneo ya Beni, Oicha, Eringeti na kwingineko huku wengi wakielezea matarajio yao kwa mwaka 2020.

“Naomba uwe ni mwaka wenye amani kwa sababu mwaka uliopita tulikuwa tunalala na kuamka bila ya amani, sasa amani irudi mwaka 2020,” alisema Deborah alipozungmza na ripota wa RFI Kiswahili Errisckson Luhembwe.

“Sisi tunachoomba ni usalama tu, bila hilo hakuna tunachoweza kufanya,” alisema Muchukunde.

Jijini Kinshasa, mwandishi wetu Freddy Tendilonge naya alishuhudia wakaazi wa jiji hilo wakiwa katika maeneo ya bustani

Ujumbe kutoka jijini Kinshasa ulikuwa ule wa amani na kutaka usalama, hasa kwa wakaazi wa Beni kwa mujibu wa wale waliofurika makanisani na maeneo mengine ya burudani.

Rais Felix Tshisekedi katika ujumbe wake wa mwaka mpya, ametoa wito wa amani huku akiahidi kuwa serikali yake itahakikisha kuwa, kila mmoja anakuwa salama hasa eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.