Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Somalia: Watano wauawa katika shambulio dhidi ya hoteli Mogadishu

Watu watano wameuawa - raia watatu na maafisa wawili wa vikosi vya usalama - katika shambulio lililotokea Jumanne usiku, Desemba 10.

Kikosi cha Umoja w Afrika nchini Somalia (AMISOM) kikipiga doria katika mji wa Mogadishu.
Kikosi cha Umoja w Afrika nchini Somalia (AMISOM) kikipiga doria katika mji wa Mogadishu. RFI/Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali wa kundi la Al Shabab dhidi ya hoteli iliyo katikati mwa mji wa Mogadishu, polisi imebaini leo Jumatano (Desemba 11) katika taarifa.

Naibu Mkuu wa jeshi la Polisi Zakia Hussein amesema, baada ya uvamizi huo uliotekelezwa na magaidi wa Al Shabab, watu 82 waliokolewa.

"Vikosi vyetu vya usalama vimezima shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya SYL (...) Idadi ya watu iwaliouawa ni watano, ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa vikosi vya usalama na raia watatu," polisi imesema, huku ikibani kwamba watu 11 wamejeruhiwa. Wanamgambo "watano" wa kundi la Al Shabab wameuawa, imesema taarifa hiyo.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa shughuli ya uzinduzi wa kitabu ilikua ikiendelea ndani ya hoteli ya SYL wakati shambulio hilo lilipotokea ambapo watu zaidi ya 70 walikua wamekusanyika kwa ajili ya tukio hilo.

Wanamgambo wa Al Shabab wamekiri kuhusika na shambulio hilo katika hoteli ya kifahari SYL mjini Mogadishu.

Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji 7 waliokua na silaha huku wakiwa wamevalia sare polisi waliingia kwenye uwanja wa hoteli hiyo na kuanza kufyatua risasi

Awali Taarifa zilisema kuwa makundi ya wanajeshi walionekana kwenye barabara inayoelekea katika ikulu ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.