Pata taarifa kuu
SUDANI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Mazungumzo ya amani kuanza tena Sudani Kusini

Mazungumzo ya amani kati ya Khartoum na waasi wa majimbo ya Sudani ya Darfur (magharibi), Kordofan Kusini (kusini) na Blue Nile (kusini-mashariki) yanatarajiwa kuanza tena leo Jumatatu katika mji mkuu wa Sudan Kusini mbele ya Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok anatarajia kushiriki mazungumzo ya amani na waasi kutoka Majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile mazungumzo ambayo yanaanza tena Jumatatu Oktoba 14 jijini Juba.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok anatarajia kushiriki mazungumzo ya amani na waasi kutoka Majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile mazungumzo ambayo yanaanza tena Jumatatu Oktoba 14 jijini Juba. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya amani nchini Sudan yanaanza Jumatatu hii (Oktoba 14) katika mji mkuu wa Sudani Kusini, Juba, na yanatarajiwa kudumu mwezi mmoja, kulingana na kile kilichofikiwa kwenye mkataba wa Septemba 11 kati ya serikali ya mpito na makundi yenye silaha.

Ni mazungumzo ya moja kwa moja lakini ya wazi na makundi mawili makubwa yenye silaha.

Sudan imejipa miezi sita kufikia mkataba kamili. Kupata amani ya kudumu nchini Sudani ni kipaumbele cha serikali ya mpito, kama alivyobaini mara kadhaa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok. Kwa hivyo hii ni hatua ya kwanza katika mazungumzo ambayo yanapaswa kufikia amani kamili ya kudumu nchini Sudani.

Viongozi wengine wakiwemo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, rais Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni, wanatarajiwa pia kuhudhuria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.