Pata taarifa kuu
SUDANI-MAREKANI-HAKI

Marekani yaweka vikwazo dhidi ya mkuu wa idara ya ujasusi wakati wa utawala wa al-Bashir

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeweka vikwazo dhidi ya Salah Gosh, mkuu wa idara ya ujasusi wakati wa utawala wa Omar Hassa al-Bashir kwa "kuhusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Sudani."

Salah Gosh, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi wa wakati wa utawala wa Omar al-Bashir, amepigwa marufukuy kuingia nchini Marekani.
Salah Gosh, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi wa wakati wa utawala wa Omar al-Bashir, amepigwa marufukuy kuingia nchini Marekani. © ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, Jumatano, Agosti 14. Salah Gosh alikuwa mkuu wa NISS, idara ya ujasusi ya Sudani katika utawala wa Omar al-Bashir. Alijiuzulu Aprili mwaka jana, siku chache baada ya Omar al-Bashir kutimuliwa madarakani. Anashutumiwa na mashirika ya haki za binadamu kuhusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, hasa mauaji ya wapinzani na wakosoaji wa Omar al-Bashir.

Salah Gosh, mkewe na binti yake sasa wamepigwa marufuku kuingia Marekani. Vikwazo vilivyothibitishwa na duru za kuaminika kutokana na kuhusika kwake katika kesi za mateso, Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani imeeleza katika taarifa yake.

Salah Gosh, ambaye pia anashtumiwa na shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Human Right Watch kuangamiza jamii katika eneo la Darfur, alikuwa mkuu wa NISS tangu mwaka 1999 hadi mwaka 2009, nafasi ambayo alishikilia tena mnamo mwaka 2018.

Baada ya kujiuzulu kwake mnamo mwezi Aprili mwaka huu, Amnesty International ilitaka mamlaka ya mpito kuchunguza kuhusika lkwake katika vifo vya waandamanaji kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.