Pata taarifa kuu
NIGER-UCHAGUZI-SIASA

Mvutano waibuka kuhusu sheria mpya ya uchaguzi Niger

Wabunge wa upinzani nchini Niger, wanapinga sheria mpya kuhusu uchaguzi ambazo zilipitishwa na bunge juma hili, wakisema zinaenda kuminya wigo wa demokrasia.

Makao makuu ya Bunge la Niger.
Makao makuu ya Bunge la Niger. Naija news
Matangazo ya kibiashara

Mwanzoni mwa juma hili, wabunge wa chama tawala waliunga mkono mapendekezo ya serikali kuhusu kufanyia marekebisho sheria za uchaguzi nchini humo lakini wabunge wa upinzani walisusia.

Kubwa hasa linalo leta utata katika sheria huyo mpya ni kipengele nambari 8 cha sheria hiyo ambacho hakimpi nafasi mpinzani Hama Amadou kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Upande wake Naibu spika wa bunge Iro Sani amesema siasa za kusususia vikao, hazijawahi kutatua matatizo ya kijamii hata siku moja, na kwamba upinzani kwa sasa unatapatapa na kutafuta pakutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.