Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-URAIS-UCHAGUZI

Kamati: Uchaguzi Mkuu wa Julai 4 hautawezekana nchini Algeria

Kamati maalum inayosimamia mchakato wa Uchaguzi Mkuu nchini Algeria inasema kuwa nchi hiyo haiwezi kufanya uchaguzi wake mkuu uliopangwa kufanyika Julai 4 mwaka huu kama ambavyo ilikuwa imekubaliwa.

Waandamanaji nchini Algeria wakiandamana kushinikiza mabadliko ya uongozi nchini humo
Waandamanaji nchini Algeria wakiandamana kushinikiza mabadliko ya uongozi nchini humo REUTERS/Ramzi Boudina shoul
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya kamati hiyo ya katiba imesema kuwa suala hili sasa linabaki mikononi mwa rais kupanga tarehe nyingine.

Tangazo hili tayari limeibua hofu ya kutokea maandamano zaidi baada ya yale yaliyosababisha rais Abdeleaziz Bouterflika kujiuzulu.

Tangu kuondolewa madarakani kwa rais Bouterflika, nchi hiyo imeendelea kushuhudia maandamano mfululizo, wananchi wakitaka kujiuzulu kwa viongozi waliohudumu chini ya utawala wake.

Tarehe 22 mwezi Februari, maelfu ya watu walianza kuandamna jijini Algiers na miji mingine kupinga hatua ya Bouteflika kutangaza kuwania tena urais kwa muhula wa tano baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 20.

Bouteflika mwenye umri wa miaka 82, aliyekuwa anasumbuliwa na kiharusi tangu mwaka 2013 alikuwa hajawahi kuonekana hadharani kwa kipindi kirefu.

Siku moja baada ya kurejea nyumbani akitokea Uswisi alikokuwa ameenda kupata matibabu, Bouteflika tarehe 11 mwezi Machi alitangaza kutowania tena urais.

Baada ya shinikizo za wananchi na baadaye jeshi kuingilia kati, tarehe 2 mwezi Aprili, Bouteflika alitangaza kujiuzulu kama rais wa nchi hiyo, hatua ambayo iliwafurahisha raia wa taifa hilo la Afrika Kaskazini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.