Pata taarifa kuu
DRC,MAWASILIANO-JAMII-USALAMA

Kampuni ya mawasiliano ya Airtel yaingia matatani mashariki mwa DRC

Wanahrakati 11 wa vuguvugu la kisiasa la Lucha wamejeruhiwa baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kukabiliana na polisi mjini Goma, wakishinikiza kampuni ya mawasiliano ya Airtel lisaidie kutokomeza utekaji nyara katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Wanaharakati wa  LUCHA (Struggle for Change) wakiandamana Kinshasa.
Wanaharakati wa LUCHA (Struggle for Change) wakiandamana Kinshasa. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wanaharakati hao wa LUCHA wamesema wataendelea kuandamana hata kama watateswa na au kufanyiwa vitisho na vikosi vya usalama.

“Mimi na wengine tutaendelea kuandamana, hatutachoka kwani

mashirika ya mawasiliyano yanatutesa sana kuhusu bei ya mawadiliano na kuwarahisisha wanao endesha utekaji nyara ,hatuta kubali kabisa, ” amesema Rebeka Kabuo, mmoja wa wanaharakati wa LUCHA.

Mashirika yanayotea haki za binadamu nchini DRC wamelaani vikali hatua ya polisi ya kuwanyima haki ya kuandamana wanaharakati hao wa Lucha.

“Tunalaani kabisa kitendo hicho cha kikatili kilichoendeshwa dhidi ya vijana

hao waliopeleka malalamiko ya raia mbele ya viongozi wa Airtel. Tunaomba Airtel wajirekebishe na wasikie malalamiko ya wananchi, “ amesema Placide Nzilamba, mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu mashariki mwa DRC.

Kampuni ya mawasiliano Airtel jijini Goma, halijazungumza chochote dhidi ya madai hayo ya LUCHA na watetezi wa haki za binaadam jijini humo.

Raia kwa upande wao wamelitaka shirika la mawasiliano la Airtel kusikiliza malalamiko ya Lucha nakuyatafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.