Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA

Uchaguzi Afrika Kusini: Upinzani wapaza sauti dhidi ya ANC

Wananchi wa Afrika Kusini wanajiandaa kumchagua rais wao mpya ndani ya wiki moja. Uchaguzi utafanyika Jumatano wiki ijayo. Rais anaye maliza muda wake Cyril Ramaphosa, anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF, mara nyingi hutumia maneno ya uchokozi dhidi ya chama tawala cha ANC anapoimba "- Kill the Boer-", Mei 1, 2019.
Julius Malema, kiongozi wa chama cha EFF, mara nyingi hutumia maneno ya uchokozi dhidi ya chama tawala cha ANC anapoimba "- Kill the Boer-", Mei 1, 2019. © REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na uchunguzi wa awali chama tawala cha ANC kinaongoza kwa 50% ya kura.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance kinasema, iwapo kitashinda uchaguzi huo, kitatekeleza maoni ya rais wa kwanza mweusi Nelsom Mandela, aliyetaka nchi ya Afrika Kusini kumjumuisha kila mmoja.

Uongozi wa chama hicho unasema kuwa, sera zao zinaangazia yale aliyoyaamini Mandela na unashtumu chama tawala cha ANC kinachopewa nafasi kubwa kwenye uchaguzi kuwa, kimeshindwa kusimamia maoni ya kiongozi huyo wa zamani.

Kwa upande wake Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha EFF, ameshtumu chama tawala cha ANC kuwatelekeza wakaazi wa vijijini.

Siku ya Jumatano alipofika katika uwanja wa Alexandra Stadium, Julius Malema alisema: "ANC ilifanya nini? Hakuna! Walijhusisha tu na kuiba fedha. Hii ndiyo sababu chama cha EFF kinasema kwamba nilazima tuwanyang'anye mashamba wakulima bila fidia na kuwapa wenyeji wa Alexandra ili waweze kujenga nyumba zao. "

Uchaguzi huu unaonekana kuwa na ushindani, lakini rais anaye maliza muda wake Cyril Ramaphosa anapewa nafasi ya kushinda uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.