Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Sudan: Polisi yatoa wito wa kutoingilia kati dhidi ya waandamanaji

Maelfu ya waandamanaji wameendelea kukusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi katikati mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum, kwa siku ya tano mfululizo.

Waandamanaji wakikusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum, tarehe 9 Aprili 2019.
Waandamanaji wakikusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum, tarehe 9 Aprili 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Desemba mwaka jana, waandamanaji wanaendelea kuomba rais Omar al-Bashir ajiuzulu, Siku ya Jumamosi waandamanaji walifaulu kufika kwenye makao makuu ya jeshi na kupiga kambi katika eneo hilo.

Kwa sasa ni maelfu ya waandamanaji ambao wanaendelea kupiga kambi mchana na usiku mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Mapema wiki hii waandamanaji walitoa wito kwa jeshi kuwaunga mkono kwa lengo la kuondoa utawala wa kiimla wa rais Omar al-Bashir.

Watu saba waliuawa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi. Kwa mujibu wa mashahidi watu 20 ndio wameuawa tangu Jumamosi wiki jana.

Waandamanaji wanataka kuundwa kwa serikali ya mpito, suala ambalo sasa mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, Norway na Uingereza yanaunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.