Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Ramtane Lamamra: Bouteflika atakabidhi madaraka kwa njia ya "uwazi"

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane Lamamra ambaye yuko ziarani nchini Urusi amesema rais Abdelaziz Bouteflika atakabidhi madaraka kwa mrithi wake kwa njia ya "uwazi" baada ya uchaguzi ambao "tarehe itatangazwa hivi karibuni".

Maandamano dhidi ya uamuzi wa rais Abdelaziz Bouteflika wa kuahirisha uchaguzi na kuongeza muda wa muhula wakewa nne, Algiers Machi 15, 2019.
Maandamano dhidi ya uamuzi wa rais Abdelaziz Bouteflika wa kuahirisha uchaguzi na kuongeza muda wa muhula wakewa nne, Algiers Machi 15, 2019. © REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

"Bouteflika aliamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi huo na yuko tayari kukabidhi madaraka kwa njia ya uwazi kwa rais atakaye chaguliwa kupitia uchaguzi," amesema Ramtane Lamamra baada ya mkutano na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.

"Uchaguzi wa urais utafanyika katika mazingira mapya: kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, watashiriki katika uchaguzi huo wale wote ambao wanataka," ameomngeza Bw Lamamra, kwa mujibu wa maneno yaliyotafsiriwa kwa Kirusi, na kuongeza kwamba uchaguzi "kwa mara ya kwanza utasimamiwa na tume huru ya uchaguzi".

"Baada ya hapo, upinzani wa Algeria utachukuwa na nafasi ya kuongoza kwa sehemu moja katika shughuli za serikali," Bw Lamamra amesema.

Abdelaziz Bouteflika, mwenye umri wa miaka 82, ambaye yuko madarakani kwa miaka 20 sasa, anakabiliwa na maradhi ya kiharusi ambayo yamemzuiwa tangu mwaka 2013 kuhutubia kwa sauti yake wananchi wa taifa la Algeria. Bouteflika anaendelea kuelemewa na maandamano ya kila siku yaliyoanza wiki kadhaa zilizopita.

Wiki iliyopita alijiondoa kwenye kunyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais na kufuta nia yake ya kuwania muhula wa tano, lakini aliamua kuongeza muda wa muhula wake, bila hata hivyo kutarajia na kusogeza mbele uchaguzi wa urais uliotarajiwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu.

Sergei Lavrov amesema kuwa "anaunga mkono" mpango wa serikali ya Algeria wa kuondokana na mgogoro huo. "Tuna imani kwamba wanasaidia kutuliza hali katika nchi hii rafiki kwa njia ya mazungumzo ya kitaifa kulingana na katiba," Bw Lavrov ameongeza.

Urusi ni mshirika a Algeria na imekuwa ikiipa msaada wa silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.