Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria: Waziri Mkuu aahidi kuundwa kwa serikali wiki ijayo

Maandamano nchini Algeria yanaendelea dhidi ya kuongezwa kwa muhula wa nne wa Abdelaziz Bouteflika. Hali hiyo inakuja, siku chache baada ya rais Ambdelaziz kutangaza kwamba amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais.

Waziri Mkuu wa Algeria Noureddine Bedoui.
Waziri Mkuu wa Algeria Noureddine Bedoui. © RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Algeria alitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu uliokuwa ulipangwa kufanyika Aprili 18. Leo Alhamisi, Waziri Mkuu mpya Noureddine Bedoui ametangaza kwamba serikali mpya itaundwa wiki ijayo.

Noureddine Bedoui ameelezea kwamba serikali itaundwa na watu kutoka tabaka mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vijana, wanawake na mashirika ya kiraia.

Amerejelea kauli yake na kusema kuwa milango imefunguliwa kwa upande wa upinzani. Waziri Mkuu amesema kuwa mamlaka wamesikia madai ya vijana wa Algeria

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.