Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Bouteflika asalimu amri kufuatia maandamano

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, amesema kuwa hatagombea tena urais kwa muhula wa tano nchini humo, hatua inayokuja baada ya taifa hilo kushuhudia maandamano ya nchi nzima kwa wiki kadhaa sasa.

RAis wa Algeria Abdelaziz Bouteflika.
RAis wa Algeria Abdelaziz Bouteflika. AFP/Eric FEFERBERG
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa urais uliotakiwa kufanyika tarehe 8, mwezi wa April na sasa umesogezwa mbele.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Algeria Ahmed Ouyahia amejiuzulu, na nasafi yake kuchukuliwa na waziri wa mambo ya ndani Noureddine Bedoui ambaye amepewa jukumu la kuunda serikali mpya.

Kwa upande wao, wapinzani wamekaribisha hatua hiyo ya rais Abdellaziz Boutteflika.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari siku ya Jumatatu, Ikulu ya rais mjini Algeirs imefahamisha kwamba tarehe mpya ya uchaguzi haijatajwa bado, na kwamba baraza la mawaziri litafanyiwa mabadiliko hivi karibuni.

Rais Bouteflikha ameiongoza Algeria kwa miaka 20 sasa, lakini hajaonekana muda mrefu mbele ya umma na maeneo mengine, kutokana na ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.