Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Algeria: Ramtane Lamamra aahidi kuwa uchaguzi utakuwa huru

Kufuatia tangazo la rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika la kutowania muhula mpya wa uongozi katika uchaguzi wa urais ujao na kuahirishwa kwa uchaguzi wa Aprili 18, Waziri Mkuu Ahmed Ouyahia amejiuzulu.

Naibu Waziri Mkuu mpya wa Algeria Ramtane Lamamra ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje mnamo mwezi Mei 2017
Naibu Waziri Mkuu mpya wa Algeria Ramtane Lamamra ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje mnamo mwezi Mei 2017 TOBIAS SCHWARZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nafasi yake imechukuliwa na Noureddine Bedoui, waziri wa zamani wa mambo ya ndani, ambaye atahusika na kuunda serikali mpya, na Ramtane Lamamra, waziri wa zamani wa mambo ya nje, ambaye ameteuliwa kuwa naibu waziri mkuu. Uchaguzi wa urais utafanyika baada ya mkutano wa kitaifa. Ramtane Lamamra amesema na kuahidi kuwa uchaguzi huru utafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

"Sasa ni kwa wanawake, wanaume na hasa vijana wa nchi hii kuongeza juhudi katika hatua hii ya kihistoria, tusitupiane makosa. Naamini kuwa kwa pamoja tutajenga nchi yetu, " amesema Ramtane Lamamra, naibu waziri mkuu mpya wa Abdelaziz Bouteflika, akihojiwa na mwandishi wa RFI Christophe Boisbouvier.

Uamuzi wa rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika wa kujiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais umekuja baada ya mfululizo wa maandamano ya nchi nzima kwa wiki kadhaa sasa.

'Hakutakua na muhula wa tano'' ilisema taarifa kutoka kwa Rais Bouteflika, ''hakuna maswali katika hilo, ukizingatia hali yangu ya kiafya, na umri wangu, kazi yangu ya mwisho kwa watu wa Algeria ni kuhakikisha wanapata uongozi mpya'' ameendelea kusema katika taarifa yake.

Ameongoza Algeria kwa miaka 20 sasa, lakini hajaonekana muda mrefu katika maeneo ya wazi , kutokana na ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2013.

Tarehe mpya ya uchaguzi haijatajwa bado, mabadiliko katika baraza la mawaziri yatafanyika hivi karibuni, taarifa iliyotolewa kwa niaba ya Bouteflika imetoa maelezo hayo.

Kwa mara ya mwisho alionekana akihutubia Umma mwaka 2014 -hotuba ya shukrani kwa raia wa Algeria kwa kuuamini utawala wake baaa ya kushinda uchaguzi uliokuwa umetangulia.

Aliahidi kutekeleza suala la mgawanyo wa madaraka, kuupa nguvu upinzani na kuhakikisha haki za raia zinafuatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.