Pata taarifa kuu
DRC-GIZENGA-JAMII

DRC yaomboleza kifo cha waziri mkuu wa zamani Antoine Gizenga

Waziri mkuu wa zamani wa DRC Antoine Gizenga amefariki dunia tangu Jumapili asubuhi akiwa na umri wa miaka 93. Taarifa ya kifo chake imetolewa na makada wa chama chake cha PALU na kuthibitishwa na serikali ya DRC.

Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Patrice Lumumba aliyeuawa mwaka 1961, mwaka mmoja baada ya uhuru, Antoine Gizenga aliendelea kuonekana kama mrithi wake wa kiroho akiongoza chama cha Palu.
Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Patrice Lumumba aliyeuawa mwaka 1961, mwaka mmoja baada ya uhuru, Antoine Gizenga aliendelea kuonekana kama mrithi wake wa kiroho akiongoza chama cha Palu. © LIONEL HEALING / AFP
Matangazo ya kibiashara

Antoine Gizenga, waziri mkuu wa Joseph Kabila kati ya mwaka 2006 na 2008, wakati wa muungano kati ya chama cha tawala (PPRD) na Palu, alikuwa pia naibu waziri mkuu kati ya mwaka 1960 na 1961.

"Tupo katika huzuni," amesema Willy Makiashi, mbunge wa taifa kutoka chama cha PALU, ambaye amekaribisha mchango wa Antoine Gizenga katika ujenzi wa DRC tangu ilipojipatia uhuru mnamo mwaka 1960.

Kwa upande wake Bob Kabamba, profesa wa sayansi za siasa katika Chuo Kikuu cha Liège nchini Ubelgiji, anasema Antoine Gizenga aliweka mbele umoja wa raia wa DRC kama moja ya vita vyake vikuu.

Gizenga alikuwa ni miongoni mwa washirika wa karibu wa muasisi wa
taifa hilo Patrice Emery Lumumba na mwenyekiti wa chama cha PALU
kilichofanya kila jitihada kuendeleza nia aliyokuwa nayo Lumumba
kuhakikisha DRC inakuwa ni taifa lenye udemokrasia na maendeleo.

Antoine Gizenga ni mmoja wa watetezi walio kuwa kwenye mstari wa mbele wa vita vya kumuunga mkono Patrice Lumumba, na alikuwa miongoni mwa wanamapinduzi ambao waliongoza mapinduzi katika miaka ya 1960 nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.