Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Jeshi lalaumiwa kwa kusababisha vifo Zimbabwe baada ya Uchaguzi Mkuu

Tume iliyokuwa inachunguza machafuko ya kisiasa, baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe mwisho wa mwez iJulai, mwaka huu, imebaini kuwa jeshi lilitumia nguvu kupitia kisiasa dhidi ya waandamanaji wa upinzani na kusababisha vifo vya watu sita jijini Harare.

Umati wa wafuasi wa upinzani wa Movement for Democratic Change MDC) wakijibu baada ya askari kuwarushia risasi mbele ya makao makuu ya chama hicho, Harare, Zimbabwe Agosti 1, 2018.
Umati wa wafuasi wa upinzani wa Movement for Democratic Change MDC) wakijibu baada ya askari kuwarushia risasi mbele ya makao makuu ya chama hicho, Harare, Zimbabwe Agosti 1, 2018. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe aliongoza tume hiyo huru, ambayo imeongeza kuwa jeshi halikuwa na sababu yoyote ya kutumia nguvu hiyo.

Hata hivyo, imewalaumu baadhi ya wanasiasa wa upinzani kuwachochea wafuasi wao kwenda kuandamana kupinga ushindi wa rais Emmerson Mnangangwa.

Rais Mnangangwa amesma ameridhika na kazi ya Tume hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.