Pata taarifa kuu
GABON-SIASA-AFYA

Katiba yafanyiwa marekebisho Gabon, upinzani walalama

Mahakama ya Katiba nchini Gabon imefanya marekebisho ya Katiba itakayotumika kwa kipindi chote rais wa nchi hiyo Ali Bongo Ondimba atakuwa bado hajarejea nchini.

Marie-Madeleine Mborantsuo, Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Gabon.
Marie-Madeleine Mborantsuo, Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Gabon. http://www.cour-constitutionnelle.ga
Matangazo ya kibiashara

Ali Bongo Ondimba amelazwa hospitali kwa wiki tatu sasa katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Upinzani na vyama vya kiraia vinaesema kuwa uamuzi huo wa Mahakama ya Katiba ni jambo "lisilo kubalika" na inaonekana kuwa ni njama za kuendelea "kuvunja sheria".

Siku ya Jumatano usiku, Marie-Madaleina Mborantsuo, Mkuu wa Mahakama ya Katiba tangu mwaka 1991, aliitisha vyombo vya habari ili kutoa taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Katiba wa kurekebisha sheria mama itakayotumika kwa kipindi chote rais Bongo atakuwa bado hajarehjea nchini.

Ali Bongo Ondimba amelazwa hosptali tangu Oktoba 24 nchini Saudi Arabia ambapo, kwa mujibu wa ofisi ya rais huko Libreville, ameanza kupata nafuu kufuatia "uchovu", "kizunguzungu" na "kutokwa na damu."

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu ugonjwa wa Ali Bongo, mwenye umri wa miaka 59, wala tarehe ya kurudi nchini Gabon kuendelea na majukumu yake.

Kwa kuwa Katiba ya sasa haielezi nani anaweza kurejelea nafasi ya rais kwa kipindi chote atakuwa hayupo, Mahakama, baada ya kuombwa na Waziri Mkuu Emmanuel Issoze Ngondet, imeamua kufanya marekebisho hayo.

"Ikiwa rais atakuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa muda kutokana na sababu mbalimbali, Makamu wa rais au Waziri Mkuu wanaweza kushikilia baadhi ya majukumu kwa idhini maalum ya Mahakama ya Katiba, " Marie-Madeleine Mborantsuo amesema.

Kama hatua ya kwanza, Mahakama ya Katiba imemruhusu Makamu wa Rais Pierre-Claver Maganga Moussavou "kuandaa na kusimamia vikao vya Baraza la Mawaziri".

Hakuna vikao vya Baraza la Mawaziri ambavyo vimefanyika tangu Rais Ali Bongo alazwe hospitali nchini Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.