Pata taarifa kuu
DRC-UNSC-SIASA-USALAMA

UNSC yatoa wito wa mazungumzo kuhusu mashine za kupigia kura DRC

Ujumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umekamilisha ziara yake ya siku mbili jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Lakini seriali ya DRC imesema haiko tayari kupokea msaada wa aina yoyote kutoka Monusco.

Balozi wa Ufaransa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, François Delattre (picha ya kumbukumbu).
Balozi wa Ufaransa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, François Delattre (picha ya kumbukumbu). JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara yao hiyo, mabalozi 15 wa baraza hilo walikutana na rais Joseph Kabila, wagombea wa urais, lakini pia Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi CENI, Corneille Nangaa, Lengo Ikiwa ni kupata mwangaza kuhusu mchakato wa uchaguzi utakaofanyika tarehe 23 mwezi Desemba mwaka huu.

Masuala yote yalijadiliwa, hata yale yanayoonekana kuzua mvutano mkubwa, wanachama wa ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamesema.

Ujumbe huo umetoa wito wa kupatikana kwa mwafaka kuhusu matumizi ya mashine za kupigia kura, lakini pia kuhusu mapendekezo mengine yaliyotolewa na wapinzani nchini Humo.

Hata hivyo serikali ya DRC imeendelea na msimamo wake wa kufutilia mbali msaada wa aina yoyote kutoka Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (Monusco).

Katika miezi ya hivi karibuni, uhusiano kati ya Joseph Kabila na Umoja wa Mataifa umeendelea kudoroa.

Rais Joseph Kabila amerejealea kauli yake kwamba yuko tayari kufadhili uchaguzi huu bila msaada wa kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.