Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-USALAMA-SIASA

Unicef: Watoto nusu milioni wako katika "hatari" Tripoli

Takriban wato 500,000 nchini Libya wako katika "hatari" katika mji wa Tripoli, ambao unakabiliwa na makabiliano mabaya kwa mwezi mmoja sasa, shirika la Umoja wa Mataifa kwa watoto (Unicef) limebaini.

Mazishi ya waathirika wa mashambulizi ya anga Sorman, Libya, Juni 22, 2011.
Mazishi ya waathirika wa mashambulizi ya anga Sorman, Libya, Juni 22, 2011. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia tarehe 27 Agosti, mapigano kati yamakundi hasimu yameuwa watu zaidi ya 115 na karibu 400 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa ripoti ya mwisho ya Wizara ya Afya iliyochapishwa siku ya Jumamosi usiku.

Mapigano yameongezeka ndani ya saa 48 Kusini mwa Tripoli na "watoto zaidi ya nusu milioni wako katika hatari" katika mji mkuu wa Libya , Unicef imesema, huku ikiongeza kwamba wako "milioni 2.6 wanaohitaji msaada nchini kote".

Mapigano ya hivi karibuni yamesababisha familia 1,200 kuhama makazi yao, na hivyo kukamilisha idadi ya wakimbizi wa ndani 25.000, kwa mujibu wa Unicef.

Nusu ni watoto, imebaini Unicef, ambayo ina wasiwasi ya kuwepo kwa "idadi kubwa ya visa vya ukiukwaji wa haki za watoto" ambavyo wanakabiliana na vyo hukoTripoli.

Pamoja na uhaba wa maji, chakula na umeme, watoto nchini Libya wanakabiliwa na tishio la ugonjwa wa Surua, ikiwa ni pamoja na kesi 500 ambazo zimejulikana, mkurugenzi wa Unicef katika kanda ya Afrika Mashariki na Kaskazini, Geert Cappelaere.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.