Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA

Serikali ya Mali yatangaza tarehe ya uchaguzi wa wabunge

Serikali ya Mali imetangaza tarehe ya uchaguzi ujao wa wabunge. Duru ya kwanza ya uchaguzi itafanyika tarehe 28 Oktoba na duru ya pili mnamo Novemba 18.

Raia huyu anajiandaa kupiga kura katika kituo cha uchaguzi cha mjini Bamako katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Mali Agosti 12, 2018 (picha ya kumbukumbu).
Raia huyu anajiandaa kupiga kura katika kituo cha uchaguzi cha mjini Bamako katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Mali Agosti 12, 2018 (picha ya kumbukumbu). ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo ambalo linakuja siku chache baada ya Ibrahim Boubacar Keita kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Agosti 12, hali ambayo ilizua mgogoro wa baada ya uchaguzi.

Katika taarifa iliyotumwa Jumanne kwa jumuiya ya kimataifa, upinzani unasema kuna kesi za wafuasi wake wanaoendelea kukamatwa nchini humo.

Tarehe hiyo ya uchaguzi wa wabunge ilitangazwa na baraza la mawaziri Jumanne wiki hii, kikao ambacho kiliongozwa na Waziri Mkuu, Soumeylou Boubèye Maïga. Na kulingana na sheria, kampeni ya uchaguzi ya duru ya kwanza ya uchaguzi itafanyika kuanzia Oktoba 6 hadi 26.

Tangazo hili linakuja katika mazingira ya kutatanisha, baada ya kiongozi wa upinzani Soumaila Cisse kushindwa katika uchaguzi wa urais kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Mahakama ya Katiba.

Soumaïla Cissé, anasema uchaguzi wa urais uligubikwa "udanganyifu mkubwa", na bado "hatambui ushindi wa Rais Ibrahim Boubacar Keita."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.