Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Shekau aonekana kwenye video baada ya uvumi kuhusu afya yake

Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau, ameonekana kwenye video kwa mara ya kwanza tangu miezi kadhaa iliyopita, wakati ambapo kulikuepo na uvumi kwamba ni mgonjwa na kuna zoezi la kumtafuta mrithi wake.

Watu wanashtumiwa kuwa na uhusiano na Boko Haram wakamatwa Maiduguri, Julai 18, 2018, Nigeria.
Watu wanashtumiwa kuwa na uhusiano na Boko Haram wakamatwa Maiduguri, Julai 18, 2018, Nigeria. REUTERS/Ahmed Kingimi
Matangazo ya kibiashara

Video hiyo ya dakika 36, iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP, inamuonyesha Shekau akikaa chini, huku akibebelea silaha aina ya Kalashnikov kwenye mkono wake wa kulia.

Shekau amesema video hiyo ilirekodiwa Julai 12 kwa ombi la wafuasi wake kwa ajili ya "kusherehekea Eid (siku kuu ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan) na kuonyesha kuwa ndugu zao wanaendelea vizuri, tofauti na madai ya watu wasio kuwa na imani.

Hata hivyo kiongozi huyo hajatoa maelezo kuhusu hali yake ya afya.

Mwishoni mwa mwezi Juni, vyanzo kadhaa vya kuaminika vilibaini kwamba kulikuepo na mazungumzo kati ya Shekau na maafisa wake wakuu kuhusu uwezekano wa kumtafuta mrithi wake, kutokana na afya yake inayoendelea kuzorota.

Kwa mujibu wa vyanzo hivi, Shekau ana matatizo ya shinikizo la damu na matatizo ya ugonjwa wa kisukari, na yote hayo yanasababisha maafisa katika kambi yake kuwa na wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kuongoza kundi hilo la Boko Haram.

Katika miaka ya hivi karibuni, Shekau alionekana mara kwa mara katika video za propaganda, lakini kuonekana kwake kwa mara ya mwisho mbele ya kamera ilikuwa Februari 6, katika video iliyodumu dakika 14 ambapo alidai kuwa kundi lake ndilo lilihusika na mashambulizi katika Jimbo la Borno (kaskazini mashariki mwa Nigeria).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.