Pata taarifa kuu
DRC-AJALI

Watu zaidi ya 50 wafariki baada ya meli kuzama magharibi mwa DRC

Maiti zaidi ya hamsini zimeopolewa baada ya meli moja kuzama Jumatano wiki hii katika mto mmoja kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Mnamo mwezi Februari, watu zaidi ya kumi na nne walikosekana katika ajali ya meli mbeli zilizozama katika Mto Congo.
Mnamo mwezi Februari, watu zaidi ya kumi na nne walikosekana katika ajali ya meli mbeli zilizozama katika Mto Congo. AFP/Junior D.Kannah
Matangazo ya kibiashara

"Ajali hii ilitokea usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, tuligundua miili 49 siku ya Alhamisi na mwili mwingine umeonekana Ijumaa hii asubuhi," Richard Mboyo Iluka, naibu gavana wa jimbo la Tshuapa (magharibi) ameliambia shirika la habari la AFP.

Ajali hiyo ilitokea kwenye mto Momboyo katika eneo la Monkoto, kilomita 750 kutoka Mbandaka, mji mkuu wa mkoa jirani wa Equateur.

Meli hiyo ya mtu binafsi ilikuwa ikifanya safari ya Mbandaka-Monkoto, huku ikiwa na abiria zaidi ya 50 na kiasi kikubwa cha bidhaa, kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na AFP.

"Sababu za ajali hiyo na idadi ya watu ambao hawajapatikana haijajulikana. Ujumbe kutoka kwa serikali ya mkoa huo tayari umetumwa katika eeneo la tukio kujua hali halisi ya mambo," Bw Mboyo ameongeza.

Ajali kama hii zinatokea mara kwa mara nchini DRC, kwenye maziwa au kwenye mito, na ajali hizi mara nyingi zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi.

Mnamo mwezi Februari, watu zaidi ya kumi na nne walikosekana katika ajali ya meli mbeli zilizozama katika Mto Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.