Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-AJALI

Watu zaidi ya 20 wapoteza maisha katika ajali ya gari Kikwit

Watu 25 wamepoteza maisha na wengine 57 kujeruhiwa, baada ya kutokea kwa ajali ya basi la abiria Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Raia na viongozi mbalimbali wakiangalia kaburi walikozikwa waathirika wa ajali ya lori la mafuta nchini DRC, Julai 3, 2010.
Raia na viongozi mbalimbali wakiangalia kaburi walikozikwa waathirika wa ajali ya lori la mafuta nchini DRC, Julai 3, 2010. Sébastien Nemeth/RFI
Matangazo ya kibiashara

Meya wa mji wa Kikwit Leonard Mutangu, amethibitisha kutokea kwa ajali hii na kusema kuwa basi hilo lilikuwa linakwenda jijini Kinshasa.

Aidha, amesema kuwa kumekuwa na uhaba wa dawa kutibu majeruhi wengi katika ajali hiyo.

Ajali kama hii zimekua zikitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Na kusababisha vvifo kadhaa.

Inasemekana kuwa ubovu au barabara mbaya ndizo husababisha ajali hizi.

Hata hivyo polisi ya barabarani inasema kuwa madereva ndio wamekua wakisababisha ajali hizo kutokana na kuendesh magari kwa mwendo wa kasi, huku wakibebeba mizigo na watu zaidi ya uwezo wa magari wanayoendesha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.