Pata taarifa kuu
SIERRA LEON-UCHAGUZI-SIASA

Wagombea wawili wa urais nchini Sierra Leone walalamikia matokeo ya Uchaguzi

Vyama viwili vya upinzani nchini Sierra Leone vimewasilisha malalamiko kuhusiana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika juma lililopita siku chache tu baada ya vyama hivyo kushindwa kufikisha idadi ya kura kuwawezesha kushiriki kwenye duru ya pili iliyopangwa kufanyika Machi 27.

Kandeh Yumkella, mmoja wa waliokuwa mgombea urais nchini Sierra Leone
Kandeh Yumkella, mmoja wa waliokuwa mgombea urais nchini Sierra Leone AFP PHOTO / Sam PANTHAKY
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa kitaifa The National Grand Coalition ulipata asilimia 6.9 ya kura zote wakati muungano wa vuguvugu la mabadiliko wao likipata asilimia 3.5 na sasa miungano hiyo miwili imejikuta ikitupwa nje ya debe katika uchaguzi wa duru ya pili.

Muungano wa NGC unaoongozwa na mwanadiplomasia wa zamani Kandeh Yumkella na ule wa C4C unaoongozwa na Samuel Sam-Sumana makamu wa rais wa zamani wa chama tawala, wanasema hawakuridhishwa na matokeo ya Uchaguzi wa urais na wanafikiria kwenda mahakamani.

Awali vyama hivi vilitaka kuhesabiwa upya kwa kura kwenye baadhi ya vituo lakini mpaka sasa vinasema havijapokea taarifa zozote kutoka kwa Tume ya Uchaguzi licha ya kuwa tume ilihesabu upya baadhi ya kura.

Siku ya Jumanne usiku, Kinara wa upinzani Julius Maada Bio kutoka chama cha Sierra Leone People SLPP alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 43.3 ya kura katika uchaguzi wa Machi 7 wakati mgombea wa chama tawala cha All People's Congress Samura Kamara akipata asilimia 42.7 ya kura.

Wawili hao watapambana katika duru ya pili na mshindi, kuunda serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.