Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA

Jeshi lazindua operesheni dhidi ya ugaidi Sinai, Misri

Msemaji wa jeshi la Misri ametangaza leo Ijumaa, Januari 9, kuwa jeshi la nchi hiyo limezindua operesheni kabambe dhidi ya ugaidi inayoitwa "Sinai 2018".

Askari wa Misri katika eneo la Sinai ya Kaskazini, Misri, Desemba 1, 2017.
Askari wa Misri katika eneo la Sinai ya Kaskazini, Misri, Desemba 1, 2017. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Msemaji huyo amesema operesheni hiyo itakuwa "pana" na haitahusu tu eneo la Sinai lakini pia itahusu maeneo mengine ya nchi.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi aliamuru jeshi na polisi kurejesha usalama katia eneo la Sinai ya Kaskazini ndani ya miezi mitatu. Rais Abdela Fatah al-Sisi alibaini kuwa watatumia "nguvu kali" kufikia lengo hilo.

Tangu mwaka 2013, eneo la Sinai ya Kaskazini limekuwa eneo la mgogoro kati ya Waislamu wenye msimamo mkali walioapa kushirikiana na kundi la Islamic State (IS) na vikosi vya usalama. Mashambulizi naoperesheni dhidi ya magaidi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu mbilikutoka pande zote mbili.

Mashambulizi mabaya pia yalitokea katika eneo la jangwani magharibi mwa nchi hiyo. Jeshi la Misri linatumia ndege za kivita kwa kuwalenga watu wenye silaha wanajaribu kuingia na vifaa vyao kupitia jangwa nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.