Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Watu 10 watekwa nyara Beni, DRC

Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha wameripotiwa kuwateka nyara watu zaidi ya 10 kwenye mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC kuwasaka wapiganaji wa waasi wa Uganda, ADF ambao wanatekeleza mauaji ya kiholela
Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC kuwasaka wapiganaji wa waasi wa Uganda, ADF ambao wanatekeleza mauaji ya kiholela UN Photo/Sylvain Liechti
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliotekwa ni mkurugenzi wa radio washirika wa RFI, RTGB Beni ambayo huwa inajiunga na matangazo yetu ya Kiswahili.

Mashuhuda wanasema watu hao walikuwa wamevalia sare za kijeshi ambapo baadae walitokemea na mateka wao kusikojulikana baada ya kuwapora kila walichokuwa nacho.

Makundi ya waasi wakiwemo Mai-Mai na kundi la ADF yamekuwa yakiyumbisha usalama kila uchao katika maeneo hayo kiasi kwamba hadi sasa ni vigumu kubaini wahusika.

 kundi la waasi wa Uganda linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC, limewaua mami ya watu katika maeneo mmbalimbali jirani na mji wa Beni.

Hivi karibuni jeshi la Uganda (UDF) likishirikiana na jeshi la DRC, (FARDC) liliendesha operesheni kabambe mashariki mwa DRC dhidi ya kundi hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.