Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Maandamano ya kisiasa yazuiwa nchini DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa wiki hii kushinikiza kujiuzulu kwa rais Joseph Kabila.

Felix Tshisekedi kiongozi wa muungano wa upinzani nchini DRC
Felix Tshisekedi kiongozi wa muungano wa upinzani nchini DRC REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa vyama vya upinzani ulikuwa umepanga maadamano siku ya Alhamisi, kuonesha hasira zao dhidi ya uongozi wa Kabila lakini pia kumtaka aondoke madarakani kufikia  mwisho wa mwaka huu.

Navyo vyama vinavyomuunga mkono rais Kabila, vilikuwa vimepanga kuandamana siku ya Jumanne kuunga mkono uongozi wa rais Kabila.

Hata hivyo, upinzani umesema kuwa utaendelea na maandamano waliyopanga kwa sababu ni haki yao.

“Nawaomba Wacongomani kujitokeza na kuandamana tarehe 30 mwezi Novemba 2017, ni haki yetu,” aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Yote haya yanakuja wakati huu ambapo Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 23 mwezi Desemba mwaka 2018.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.

Polisi jijini Kinshasa katika siku zilizopita, wamekuwa wakikabiliana na waandamanaji wa upinzani kwa kuwakamata na hata kuwafwatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.