Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI

Waziri Mkuu wa DRC Bruno Tshibala akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu

Bruno Tshibala, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu. Muda wa masaa arobaini na nane aliopewa ili ajiuzulu unamalizika siku ya Ijumaa usiku, Novemba 24.

Waziri Mkuu Bruno Tshibala, Aprili 4, 2017 Kinshasa.
Waziri Mkuu Bruno Tshibala, Aprili 4, 2017 Kinshasa. JUNIOR KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akiitishwa bungeni kuelezea kuhusu kucheleweshwa kwa kuwasilisha muswada wa bajeti wa mwaka 2018, jibu la Waziri Mkuu halikuridhisha wabunge.

"Ni wazi kwa kweli, Bruno Tshibala alitoa majibu sio tu yasioeleweka, lakini majibu ya uongo". Henri Thomas Lokondo na wabunge wenzake wamesema kughadahabishwa na majibu hayo.

Kuanzia Ijumaa usiku, kama Waziri Mkuu hakujiuzulu, mbunge kutoka chama tawala ameahidi kukusanya saini 125 zinazohitajika ili kumtimua Bruno Tshibala. Henri Thomas Lokondo anazungumzia tukio hilo kama ukiukwaji wa Katiba na sheria ya fedha.

Siku ya Jumatano, Waziri Mkuu alitishwa bungeni. Bruno Tshibala alitakiwa kusema kwa nini sheria ya bajeti ya mwaka 2018 iliwasilishwa siku mbili tu kabla ya kuhitimishwa kwa kikao cha bajeti. Hata hivyo, Katiba na Sheria ya Fedha vinaagiza kwamba muswada wa bajeti ulitakiwa kuwasilishwa bungeni Septemba 15 ili kuruhusu mabunge yote, bunge la Wawakili na bunge la Seneti watathmini muswada juo angalau miezi miwili.

Katika jibu lake, ambalo wabunge hao wanaona kuwa alipotosha bunge, Bruno Tshibala alielezea kuingiliana kwa bajeti za mwaka 2016 na 2017 pamoja na tathmini ya uchaguzi na kalenda ya uchaguzi ambavyo alipaswa kusubiri. Jibu hilo halikumridhisha Henri Thomas na Wabunge wenzake na hivyo kumtaka ajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.