Pata taarifa kuu
SOMALIA-UGAIDI

Idadi ya vifo vya shambulizi la Mogadishu yafikia 358

Idadi ya vifo vilivyotokana na shambulizi baya zaidi la bomu kuwahi kushuhudiwa nchini Somalia imeendelea kuongezeka na kufikia watu 358 huku zaidi ya 228 wakijeruhiwa, serikali ya nchi hiyo imefahamisha, ongezeko ambalo ni kubwa katika maafa hayo.

Eneo lilikotokea shambulizi la bomu mjini Mogadishu Somalia  tarehe 14 Oct 2017
Eneo lilikotokea shambulizi la bomu mjini Mogadishu Somalia tarehe 14 Oct 2017 REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo limedhoofisha zaidi mfumo dhaifu wa afya nchini Somalia, huku washirika wake kutoka Marekani,Qatar,Uturuki na Kenya wakipeleka vifaa vya matibabu pamoja na madaktari, ambapo wote kwa pamoja isipokuwa Marekani wakiwaokoa wengine waliojeruhiwa.

Lori lililojaa mabomu lililipuka huko Hodan mnamo Oktoba 14, na kuharibu majengo 20 katika wilaya ya kibiashara, na kuacha idadi kubwa ya waathirika wakiungua kiasi cha kushindwa kutambulika.

Wataalam kadhaa wameiambia AFP kuwa lori hilo yawezekana lilibeba takribani kilo 500 za mabomu huku Waziri wa Habari Abdirahman Osman akiandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa Idadi ya hivi karibuni ya maafa ni 642 ambapo 358 walmeuawa, 228 wamejeruhiwa, 56 hawajulikani walipo na kwamba 122 ya waliojeruhiwa wamekimbizwa Uturuki, Sudan na Kenya kupata matibabu.

Hadi sasa hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na shambulizi hilo licha ya kwamba kundi la Al Shaabab limekuwa likitekeleza mashambulizi kama hayo nchini Somalia kwa lengo la kuuondoa utawala wa Somalia lakini wadadisi wanasema kuwa kundi hilo hukaa kimya pale linapotekeleza shambulizi linalochochea hasira za umma.

Hadi sasa miili ya watu zaidi ya 100 ambao hawakutambulika tayari imezikwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.