Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

George Weah na Joseph Boakai kuchuana katika duru ya pili ya uchaguzi Liberia

Tume ya Uchaguzi nchini Liberia imetangaza kuwa, mchezaji wa zamani wa mchezo wa soka George Weah aliyeshinda mzunguko wa kwanza wa Uchaguzi wa urais, atapambana na Makamu wa rais Joseph Boakai katika Uchaguzi wa mzunguko wa pili mwezi ujao.

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Liberia umepangwa kufanyika mnamo mwezi Novemba.
Duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Liberia umepangwa kufanyika mnamo mwezi Novemba. AFP/Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Weah alishinda Uchaguzi wa mwezi huu kwa kupata ushindi kwa asilimia 38.4 akiwania kupitia chama cha Congress for Democratic Change huku Boakai, kutoka chama tawala cha Unity Party akipata asilimia 28.8.

Liberia inaelekea duru ya pili ya uchaguzi wa urais, ambapo nyota wa zamani wa soka George Weah atachuana na Makamu wa rais Joseph Boakai.

Duru ya pili kati ya wawili hao inatarajiwa mnamo mwezi Novemba.

Hatua ngumu imeanza kwa George Weah, ambaye katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2005, aliongoza kwa pointi 8 mbele ya mshindani wake wakati huo Ellen Johnson Sirleaf ambaye katka duru ya pili alishinda kwa 60% ya kura. Watu wengi wanaona kuwa huenda hali kama hiyo ikatokea katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Weah na Boakai wote walikuwa wametabiri kuwa wangeshinda duru ya kwanza.

Joseph Boakai, mwenye umri wa miaka 73, amepewa jina la "Sleepy Joe", kwa sababu mara nyingi huonekana kwenye kamera akisinzia. Ni Makamu wa rais wa Ellen Johnson Sirleaf tangu mwaka 2005.

George Weah anaungwa mkono kisiasa na mbabe wa vita aliye gerezani rais wa zamani Charles Taylor. Mke wa zamani wa Taylor Jiwel Howard, ni mgombea mwenza wa Weah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.