Mlipuko wa bomu waua watu 30 Somalia
Watu thelathini wameangamia na wengine wengi wamejeruhiwa katika mlipuko mkubwa wa bomu uliotokea karibu na lango kuu la hoteli lenye watu wengi katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia, kwa mujibu wa maafisa wa usalama.
Imechapishwa:
Polisi wanasema kuwa watu wawili waliuawa katika mlipuko mwengine wa pili katika wilaya ya Madina katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kutekeleza shambulio hilo, lakini inaaminiwa kwamba mlipuko huo ulitokea dakika chache tu baada ya lori lililoegeshwa na vilipuzi kulipuliwa karibu na lango kuu la hoteli, kwa mujibu wa polisi.
Mashambulizi mengi ya kundi la Al Shabab yamekua yakiulenga mji wa Mogadishu.
Baadhi ya mashahidi wanasema kuwa hoteli ya Safari ilianguka huku watu kadhaa wakidaiwa kukwama chini ya vifusi vyake, wakiongeza kuwa wanaamni kuwa watu wengi waliangamia katika mlipuko huo.
Aftermath of #Mogadishu blast, as viewed from British Embassy pic.twitter.com/XVXCn6A675
David Concar (@DConcar) 14 octobre 2017