Watu sita waangamia katika shambulio Mogadishu
Watu sita wamepoteza maisha katika mlipuko wa bomu lililotokea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, na wengine 10 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa vyanzo vya usalama.
Imechapishwa:
Bomu la lililotegwa katika gari lililipuka nje ya maduka katika mtaa wenye shughuli nyingi katika mji wa Mogadishu.
Wakati huo huo wapiganaji wa Al Shabaab wanasema wamewaua askari wengi wa kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM kusini mwa Mogadishu.
Lakini Msemaji wa kikosi cha askari wa Umoja wa Afrika (AMISOM) amethibitisha kuwepo kwa mapigano lakini hajasema ni wanajeshi wangapi wameuawa au kujeruhiwa katika mapigano hayo.
Usalama unaendelea kuzorota nchini Somalia kufuatia mashambulizi ya hapa na pale ya kundi la Al Shabab.