Pata taarifa kuu

Monusco haikubaliani na matumizi ya nguvu ya jeshi la DRC kwa kuzima maandamano

Tume ya Umoja wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (Monusco) imelaani matumizi ya nguvu yaliyotumiwa na jeshi la serikali, kutuliza maandamano ya wanafunzi mjini Bukavu mkoa wa kivu ya kusini.

Askari polisi katika gereza la Bukavu baada ya makabiliano na wafungwa mwaka 2012.
Askari polisi katika gereza la Bukavu baada ya makabiliano na wafungwa mwaka 2012. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo Maman Sidikou ameelezea maskitiko yake kuotokana na matumizi ya nguvu yaliotumiwa na jeshi la Serikali yaliosababisha kifo cha binti mmoja mwenye umri mtogo aliepigwa risase wakati akielekea shuleni.

Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu katika kata ya Panzi wakati vikosi vya usalama vilitumia risase katika kuwatawanya watu waliokuwa wakiandamana wakilaani kukithiri kwa usalama mdogo katika maeneo hayo.

Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeanzisha uchunguzi kubaini wahusika wa tukio hilo, na kwamba matumizi ya nguvu dhidi ya raia wa kawaida hayakubaliki na kwamba vikosi vya usalama vinaruhusiwa kutumia nguvu iwapo itashindikana kabisa.

Bw. Sidikou amesema taarifa za kwamba waandamaniji wanatumia nguvu wakati wa maandamano, sio sababu ya vikosi vya Usalama kutumia risase za moto katika kuwatawanya.

Maman Sidikou amewataka viongozi wa serikali ya DR Congo kuhakikisha wanajeshi wanaotumwa kuzima maandamano wanapewa vifaa na mafunzo ya kukabiliana na raia, pamoja na kufanya uchunguzi kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa matukio hayo, ili kukomesha vitendo vya umwagaji wa damu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.