Pata taarifa kuu
DRC

Wakimbizi 36 wa Burundi wauawa katika vurugu nchini DRC

Wakimbizi 36 wa Burundi wameuawa katika mapigano huko Kamanyola Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati wa maandamano kupinga kurejeshwa nyumbani kwa wenzao maafisa wamesema jana Jumamosi.

Mkuu wa MONUSCO nchini DRC Maman Sidikou
Mkuu wa MONUSCO nchini DRC Maman Sidikou monusco.unmissions.org
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaolinda amani nchini DRC MONUSCO, Maman Sidikou amesema katika taarifa jana Jumamosi kuwa takribani wakimbizi 36 wameuawa.

 

Polisi ya DRC inasema kuwa kati ya waliojeruhiwa wamo warundi 122, askari 6, polisi 3 na raia watatu wa DRC

 

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani Josue Boji amesema askari walijaribu kuwatawanya wakimbizi kwa kupiga risasi hewani lakini walizidiwa baada ya wakimbizi hao kujibu mashambulizi kwa kurusha mawe.

 

Makumi kwa maelfu ya raia wa Burundi walitoroka taifa hilo wakati wa ghasia za mwaka 2015 kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.