Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

CENCO yaomba kuachiwa kwa mapadri wawili waliotekwa nchini DRC

Baraza Kuu la maaskofu wa kanisa Katoliki nchini DR Congo (CENCO) limelaani kutekwa kwa mapadri wawili wa kanisa Katoliki wa Parokiya Notre-Dame des Anges de Bunyuka, dayosisi ya Beni katika mji wa Butembo, mkoa wa Kivu Kaskazini.

Mwenyekiti wa baraza hilo la kanisa Katoliki nchini DR Congo, Askofu Marcel Utembi
Mwenyekiti wa baraza hilo la kanisa Katoliki nchini DR Congo, Askofu Marcel Utembi REUTERS/Robert Carrubba
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliotolewa siku ya Jumatatu, baraza hilo limelaani vikali kitendo hicho cha utekeji nyara pamoja na hali ya usalama mdogo inayoendelea mashariki mwa Congo na hivyo kuwatolea wito viongozi wa serikali kutekeleza jukumu lao ambalo ni kuwalindia usalama wananchi wake.

Baraza hilo linamewaomba viongozi wakuu katika vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha wamewakomboa mapadri hao na kuusambaratisha mtandao unaohusika na utekaji nyara ambao unayumbisha usalama katika maeneo ya Beni.

Mbali na ombi hilo la kuwakomboa ma Padri Charles Kipasa na Jean-Pierre Akilimali, baraza hilo limevitaka vikosi vya usalama kuwakomboa pia makuhani Jean Pierre Ndulani, Edmond Kisughu na Anselme Wasukundi, waliotekwa nyara tangu mwezi Octoba mwaka 2012 katika wilaya ya Beni na ambao hadi sasa hawajaachiwa huru.

Taarifa hiyo iliosaniwa na Mwenyekiti wa baraza hilo la kanisa Katoliki nchini DR Congo, Askofu Marcel Utembi, imekumbusha kuwa makuhani ni watu wa Mungu, waliojitolea maisha yao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi bila kuwa na agenda yoyote ya kisiasa, hivyo kuwafanyia unyama ni kuathiri jamii nzima wanayohudumia.

Watu wenye silaha ambao hawajulikani bado, wamewateka mapadri Pierre Akilimali na Charles Kipasa, katika usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii katika aneo la Beni hadi sasa haijulikani walipo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.