Pata taarifa kuu
DRC-EU-VIKWAZO

Vyama vinavyomuunga mkono rais Kabila vyastumu Umoja wa Ulaya

Muungano wa Vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umeushutumu umoja wa Ulaya kwa kuingilia mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.

Rais wa DRC Joseph Kabila, ambaye anaendelea kutuhumiwa na upinzani kwamba hana nia ya kuandaa uchaguzi kwa muda uliopangwa kulingana na katiba.
Rais wa DRC Joseph Kabila, ambaye anaendelea kutuhumiwa na upinzani kwamba hana nia ya kuandaa uchaguzi kwa muda uliopangwa kulingana na katiba. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Muungano huo unaulaumu umoja wa Ulaya kwa kutangaza vikwazo dhidi ya mawaziri na maafisa wengine wa serikali kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu lakini pia kwa kushindwa kuandaa mchakato mzuri wa Uchaguzi jatika nchi hiyo.

Hayo yakijiri Olivier Kamitatu, kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani wa ARC, amejiunga rasmi na kambi ya Moise Katumbi Chapwe kama msemaji wake. Spika wa zamani wa Bunge na Waziri wa zamani wa Mipango Olivier Kamitatu, tangu mwezi Septemba 2015, ni mpinzani wa kisiasa dhidi ya rais Joseph Kabila Kabange.

"Uzoefu na utaalamu wa Olivier Kamitatu vitatusaidia sana katika mapambano yetu ya amani ya kuanzisha utawala wa sheria katika nchi yetu. Kujiunga huko kwa Olivier Kamitatu, unaleta ujumbe wa kuheshimu Katiba na kuzingatia matakwa ya wananchi. Kwa sababu tunashirikiana mawazo, kwa hiyo atakua msemaji wangu, " amesema Moise Katumbi Chapwe.

Wapinzani wa kisiasa DRC Olivier Kamitatu na Charles Mwando Nsimba
Wapinzani wa kisiasa DRC Olivier Kamitatu na Charles Mwando Nsimba THIERRY CHARLIER / AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.