Pata taarifa kuu
DRC-AFRIKA KUSINI-MUKUNGUBILA-SIASA

Afrika Kusini yatoa hifadhi ya kisiasa kwa mchungaji kutoka DRC

Mpinzani wa Rais Joseph Kabila, Joseph Mukungubila amepewa hifadhi ya kisiasa nchini Afrika Kusini. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inamshtumu kuhusika katika ghasia zilizotokea mwishoni mwa mwaka 2013.

Mchungaji Joseph Mukungubila baada ya kutokea mahakamani Johannesburg Julai 15, 2014.
Mchungaji Joseph Mukungubila baada ya kutokea mahakamani Johannesburg Julai 15, 2014. MUJAHID SAFODIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Joseph Mukungubila ambaye anajulinakana kwa jina la utani na wafusai wake la "nabii wa Bwana," ni kiongozi wa kanisa iliyojengwa hasa katika miji ya Kinshasa na Lubumbashi.

Licha ya kushindwa katika uchaguzi wa urais wa 2006, Joseph Mukungubila anaonekana kama mpinzani katika serikali ya Joseph Kabila akimsmhtumu rais wa nchi hiyo kuwa na asili ya Rwanda na uporaji wa mali asili unaofanywa na nchi jirani.

Mwisho wa mwaka 2013, watu walidai kuwa wafuasi wa Mchungaji Joseph Mukungubila walishambulia maeneo muhimu katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya redio ya taifa na televisheni. Wakati huo wafuasi wake wengi waliuawa.

Akielezea kuwa mashambulizi dhidi yake yalikua yalipangwa na serikali, Mukungubila aliitoroka nchi yake na kukimbilia nchini Afrika Kusini ambako anatafuta hifadhi ya kisiasa.

Mchungaji Mukungubila alikamatwa mara kadhaa na polisi nchini Afrika Kusini kabla ya kuachiliwa.

Kwa mujibu wa msemaji wake, ni ushindi. Mchungaji sasa yuko huru kuendelea na shughuli zake za kisiasa kutoka Afrika Kusini na hasa kuendelea kuhamasisha raia wa DRC dhidi ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.