Pata taarifa kuu
DRC_BDK-USALAMA

Kundi la Kamuina Nsapu kumpata kiongozi mpya wa jadi DRC

Kiongozi mpya wa kundi lililokua likiongozwa na Kamuina Nsapu aliyeuawa mwezi Agosti mwaka jana anatarajiwa kuteuliwa leo katika mji wa Kananga, katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani Emmanuel Shadary Ramazani akipokelewa katika mji wa Kananga na naibu Gavana wa mkoa wa Kasai ya Kati, Justin Milonga.
Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani Emmanuel Shadary Ramazani akipokelewa katika mji wa Kananga na naibu Gavana wa mkoa wa Kasai ya Kati, Justin Milonga. RFI / Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Miezi tisa iliyopita, Kamuina Nsapu aliishtumu serikali ya DRC ambayo ilikataa kumtambua. Aliuawa mwezi Agosti na tangu wakati huo vurugu zimeendelea kushuhudiwa. Watu wasiopungua 500 walipoteza maisha katika maeneo mbalimbali ya Kasai, huku watu 600 000 wakiyahama makazi yao. Naibu Waziri Mkuu kwa sasa anazuru mkoa wa Kasai kwa mara ya pili katika muda wa miezi miwili. Na majadiliano na jamii ya Kamuina Nsapu yameanza kuzaa matunda.

Kama ilivyoahidaiwa tayari zaidi ya mwezi mmoja umepita, mwili wa kiongozi Kamuina Nsapu ulikabidhiwa familia yake. Ilikuwa moja ya masharti ya ndugu, jamaa na marafiki wa kiongozi huyo wa kimila, kwanza ili kumzika kwa mujibu wa mila na kuchagua mrithi wake.

Baada ya siku mbili ya majadiliano yanayofanyika kwa siri, familia ya Kamuina Nsapu imemteua Jacques Kabeya wa Ntumba kuchukua uongozi, na alichukua nafasi hiyo akiwatolea wito wafuasi wa Kamuina Nsapu kuwa watulivu. Thomas Nkashama, ndugu wa kiongozi mpya wa kijadi, amesema machafuko hayana nafasi tena.

"Hatuwezi kusalia katika vita hii ambayo haina faida na yeyote. Kwa sababu vita vyetu vilikua na malengo kwa kuweza kutambuautawala wa Kamuina Nsapu. Kwa sababu Kamuina Nsapu si mtu yeyote. Tulitoa masharti yetu. Serikali imeanza kuyatekeleza. hivyo basi, kwa upande wetu, machafuko hayana na fasi, " amesema Thomas Nkashama.

Miongoni mwa masharti hayo kuna uwezekano wa wanamgambo wa kundi hilo kujiunga katika jeshi na polisi kama wakitaka. Naibu Waziri Mkuu, Emmanuel Ramazani Shadari, amesema hajapinga hilo.

"Wajumbe wa serikali watazuru mkoa huu wiki ijayo. Nadhani watatathmini maombi yenu. Hakuna kizuizi, " amesema Emmanuel Ramazani Shadari.

Naibu Makamu wa rais pia ametoa onyo kali kwa wale ambao wanaendelea kufanya vurugu, akibaini kwamba watachukuliwa kama magaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.