Pata taarifa kuu
SOMALIA

Rais wa Somalia atangaza vita dhidi ya Al Shabab, awataka kujisalimisha

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" ametangaza vita dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.

Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" (Katikati) akiwa na walinzi wake April 6 2017
Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" (Katikati) akiwa na walinzi wake April 6 2017 TheVillaSomalia
Matangazo ya kibiashara

Farmajo ambaye amekuwa rais kwa miezi minne, ameongeza kuwa anatoa siku 60 kwa wanamgambo hao kujisalimisha.

Amefafanua kuwa ikiwa watajisalimisha, watapewa mafunzo ya kijeshi, watapewa elimu na kuajiriwa na serikai ya Mogadishu.

Kauli hii ya kiongozi huyu wa Somalia inakuja siku moja baada ya shambulizi la bomu mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine.

Amesisitiza kuwa maafisa wa usalama wamejipanga ipasavyo kuhakikisha kuwa mashambulizi ya Al Shabab hayatokei tena na wanakabiliwa ipasavyo.

Hivi karibuni, rais Farmajo aliwabadilisha maafisa wa usalama katika idara ya ujasusi katika juhudi za kukabiliana na Al Shabab.

Rais huyo ameyasema haya mjini Mogadishu ikiwa amevalia sare za kijeshi pamoja na Waziri wake Mkuu Hassan Ali Khayre, na kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuunga mkono juhudi za wanajeshi.

Kundi la Al Shabab ambalo lilianza mashambulizi yake nchini Somalia mwaka 2006, limesababisha mamia ya watu kupoteza maisha nchini Somalia na katika nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.