Pata taarifa kuu
SUDAN

Watu 50 wauawa nchini Sudan katika mapigano ya kikabila

Watu zaidi ya 50 wameuawa katika jimbo la Kordofan nchini Sudan baada ya kuzuka kwa makabiliano makali kati ya makabila mawili ya wafugaji.

Wafugaji katika jimbo la Kordofan nchini Sudan
Wafugaji katika jimbo la Kordofan nchini Sudan Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa wafugaji hao kutoka makabila ya Hamar na Kababish, walianza kushambuliana kwa bastola kuhusu umiliki wa mifugo na kusababisha mauaji haya makubwa.

Walioshuhudia tukio hilo la Jumatatu wanasema idadi kubwa ya watu waliouawa ni kutoka kabila la Hamar ambao wanakadiriwa kuwa 30.

Hata hivyo, inaripotiwa kuwa watu wengine kutoka kabila la Kababish wakiwemo wanawake, walipoteza maisha katika makabiliano hayo.

Hii sio mara kwanza kwa wafugaji kukabiliana nchini humo hasa kutoka jimbo la Kordofan na Darfur, maeneo ambayo shughuli kubwa ya kiuchumi ni ufugaji.

Wafugaji mara nyingi hushambuliana kwa sababu ya wizi wa mifugo lakini pia maeneo ya kulisha mifugo yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.