Pata taarifa kuu
IVORY COAST

Simone Gbagbo afutiwa kesi ya machafuko ya kisiasa mwaka 2010

Mahakama kuu jijini Abidjan nchini Cote D’Ivoire imemuachilia huru Simone Gbagbo mke wa Laurent Gbagbo rais wa zamani wa nchi hiyo anayeshikiliwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC.

Simone Gbagbo (Kulia) mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo
Simone Gbagbo (Kulia) mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Kesi ya Simone imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya miezi 10 na Majaji wameamua kuwa hakuna ushahidi kuonesha kuwa alichochea kuuawa kwa rais nchini humo.

Muungano wa mashirika ya waathirika wa vurugu na machafuko ya nchini humo wamesema wamehuzunishwa na hatua hiyo na kutaka Simone afikishwe katika Mahakama ya ICC kushtakiwa na mumewe.

Mwanasheria mkuu wa serikali Ali Yee amesema, huenda uamuzi huu wa Mahakama ukawa ni ujumbe kwa wanasiasa kuelekea katika maridhiano.

Simone wakati wote alikuwa anakusha madai ya kuhusika katika machafuko na kesi hiyo ilikuwa ni ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.