Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Cote d'Ivoire yaadhimisha mwaka mmoja wa shambulio la Grand-Bassam

 Ni mwaka mmoja sasa baada ya kutokea shambulio dhidi ya hoteli ya Gran-Bassam nchini Cote d'Ivoire. Shere ya kutoa heshima kwa wahanga 19 wa Grand-Bassam itafanyika Jumatatu hii asubuhi, Machi 13.

Askari wa Cote d'Ivoire wakipiga doria katika pwani ya Grand-Bassam siku moja baada ya shambulizi, Machi 14, 2016.
Askari wa Cote d'Ivoire wakipiga doria katika pwani ya Grand-Bassam siku moja baada ya shambulizi, Machi 14, 2016. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tarehe 13 Machi, kwa mara ya kwanza, Cote d'Ivoire ilikumbwa na shambulio la kigaidi. Tangu wakati huo, uchunguzi ulifanyika kwa mafanikio makubwa, kwa msaada wa ushirikiano kati ya Idara za ujasusi za Afrika Magharibi.

Katika siku ya leo serikali ya cote d'Ivoire imewataka raia kusalia kimya kwa muda wa dakika moja ifikapo saa 12:45 mchana saa za Afrika magharibi.

Jumla ya watu 38 walikamatwa kuhusiana na uchunguzi wa shambulio la Grand-Bassam. Wengi wao walikamatwa nchini Cote d'Ivoire, lakini pia operesheni kama hiyo ilifanyika nchini Burkina Faso, Mali na Senegal.

"Tumejua wale wote wanliohusika katika shambulio la Grand-Bassam, amejipongeza Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cote d'Ivoire. Tuliwakamata viongozi waandamizi wa shambulio hilo, " Waziri huyo ameongeza.

Uchunguzi ulifanyika kwa haraka, kwa mujibu wa serikali ya Cote d'Ivoire,na tilipata mafanikio kupitia ushirikiano kati ya Idara mbalimbali za ujasusi za Afrika Magharibi lakini pia Ufaransa, Algeria na Morocco. "Ni matumaini kwa mapambano dhidi ya ugaidi," Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cote d'Ivoire amebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.