Pata taarifa kuu
NIGERIA

Nigeria: Rais Buhari arejea nyumbani asema makamu wake kuendelea kukaimu urais

Saa chache baada ya kurejea nyumbani akitokea Uingereza alikokuwa ameenda kwa matibu, rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amekutana na makamu wake wa rais pamoja na mawaziri, na kuwaeleza kuwa ataendelea kupumzika zaidi huku majukumu yake yakitekelezwa na makamu wake.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akisalimiana na askofu wa kanisa Anglikana, Justin Welby ambaye alimtembelea wakati akiwa jijini Londo. Machi 9, 2017.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akisalimiana na askofu wa kanisa Anglikana, Justin Welby ambaye alimtembelea wakati akiwa jijini Londo. Machi 9, 2017. Nigeria Presidential Office/Handout
Matangazo ya kibiashara

Rais Buhari baada ya kuwasili mjini Abuja, amesema kuwa atapenda kupata nafasi ya kupumzika zaidi na kwamba makamu wa rais, Yemi Osinbajo, ataendelea kukaimu nafasi hiyo hadi pale atakaporejea kazini.

Buhari mwenye umri wa miaka 74, na ambaye alichukua usukani kuongoza nchi hiyo mwaka 2015 mwezi Mei, aliondoka mjini Abuja Januari 19 mwaka huu, kwaajili ya matibabu nchini Uingereza.

Awali alikuwa amepanga kukaa nchini Uingereza kwa muda wa siku 10 lakini akalazimika kuongeza muda wa kukaa huko baada ya kushauriana na madaktari wake wanaomtibu, hali iliyozusha sintofahamu zaidi kuhusu afya yake.

"Rais Buhari ametoa shukrani kwa raia wote wa Nigeria wanaoishi nchini humo na nje ya nchik kwa kumuombea," imesema taarifa ya ikulu iliyotolewa Alhamisi ya wiki hii, ikiongeza kuwa kuongeza kwake muda kusalia nchini Uingereza kulitokana na ushauri wa madaktari.

Hata hivyo taarifa hii ya ikulu haikuweka wazi taarifa za kina kuhusu kilichokuwa kikimsumbua rais Buhari.

Mapema siku ya Alhamisi, idara ya habari ya ikulu ya Nigeria, ilichapisha kwenye mtandao, picha ikimuonesha rais Buhari akisalimiana na askofu mkuu wa kanisa la Anglikana Justin Welby jijini London.

Hakukuwa na picha yoyote rasmi ya mikutano ya rais Buhari aliyoifanya akiwa London, hadi picha za hivi leo Ijumaa, Machi 10.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikijaribu kufanya kila namna kuwatoa hofu wananchi wa Nigeria ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu mwenendo wa uchumi wa taifa hilo wakati rais Buhari akiwa nje ya nchi.

Makamu wa rais Yemi Osinbajo alipewa madaraka yote ya rais katika kipindi ambacho rais Buhari hakuwepo nchini, hali ambayo angalau ilituliza hofu kwa wananchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.