Pata taarifa kuu
UJRUMANI-AFRIKA-ULINZI

Jeshi la Ujerumani kwenye mstari wa mbele katika ulinzi Afrika

Jeshi la Ujerumani limeimarisha uwepo wake nchini Mali, pamoja na kuwasili kwa helikopta nane na askari kadhaa, uamuzi ambao ni ishara ya kuongezeka kwa nguvu za Ulaya ambazo Ufaransa imetoa wito kutumiwa barani Afrika.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian,  akikaribisha marubani wa jeshi la Ujerumani katika mji wa Gao, Februari 25, 2017.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, akikaribisha marubani wa jeshi la Ujerumani katika mji wa Gao, Februari 25, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, helikopta nne za uchukuzi aina ya NH90 kutoka Ujerumani ziliegeshwa kwenye uwanja wa ndege wa mjini Gao, kaskazini mwa Mali, uwanja ambao umegeuzwa kambi ya Umoja wa Mataifa na kikos cha jeshi la Ufaransa cha Barkhane, kwa lengo la kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel.

Mapema mwezi Machi zitatumwa nchini Mali helikopta zingine nne za vikita aina ya Tigerambazo zitachangia kwa kuimarisha usalama na zitashiriki katika ujumbe wa upelelezi, sambamba na magari ya kivita na ndege zisizo na rubani kutoka Ujeruman.

"Ujumbe huo wa upelelezi ni mchango wetu mkuu kwa Minusma, " ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, mkuu wa kikosi cha askari wa Ujerumani, Luteni Kanali Marc Paare ameeleza.

Idadi ya askari hao imeongezeka kutoka 150 hadi 800 katika miezi michache tu na wanatazamiwa kufikia 1,000 hivi karibuni.

"Ahadi ya washirika wa Ulaya ni muhimu. Zoezi hilo la kupelekwa kwa askari ho wa Ujerumani ni kitendo cha hiari na mshikamano kwa upand wetu, " alikaribisha Jumamosi wiki hii, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, alipozuru kikosi cha askari wa Ufaransa cha Barkhane.

Ufaransa, alioingilia kati mwaka 2013 kwa lengo la kuwatimua wanajihadi kaskazini mwa Mali, imerejelea mara kadhaa wito wa ahadi za Ulaya dhidi ya ugaidi katika eneo la Sahel, ugaidi ambao ni tishio la usalama linalosambaa hadi kaskazini ya bahari ya Mediterranean.

Kwa sasa Ujerumani ina askari 12.000 katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.