Pata taarifa kuu
MALI-EU-USHIRIKIANO

Mali: Ayrault na Steinmeier waanza ziara ya pamoja Sahel

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault na mwenzake wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier wanaanza Jumatatu hii, Mei 2 ziara ya siku mbili nchini Mali na Niger. Mawaziri hawa wamewasili katika mji wa Mali, Bamako siku ya Jumapili usiku.

Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier (kushoto) na Jean-Marc Ayrault (kulia), katika uwanja wa ndege wa Berlin.
Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier (kushoto) na Jean-Marc Ayrault (kulia), katika uwanja wa ndege wa Berlin. © Reuters/Markus Schreiber/Poo
Matangazo ya kibiashara

Wanatazamiwa kutembelea mji wa Gao kisha Niamey. Lengo la ziara hii ya pamoja, ikiwa ni ya tatu ya aina yake: inaonyesha kwamba Ulaya, Ujerumani na Ufaransa wanagawana maslahi ya kawaida katika kurejesha utulivu katika ukanda huo.

Ajenda ya siku hii ya kwanza ya ziara yao, ni pamoja na mkutano na Rais wa Mali Ibrahim Boubakar Keita (IBK). Mkutano huo ulikua ulitarajiwa Jumapili jioni lakini uliahirishwa kutokana na kuchelewa kuwasili kwa Mawaziri hao mjini Bamako. Tairi ya ndege yao ilipasuka ilipokua ikijianda kuruka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Berlin. Matokeo yake, saa tatu za kuchelewa na ajenda rasmi kusogezwa mbele kwa kiasi fulani.

Mawaziri hawa wawili wa Mambo ya Nje pia watakutana Jumatatu hii asubuhi kwa mazungumzo na mawaziri wa masuala ya Maridhiano na Utawala. Moja ya malengo ya ziara hii ni kusaidia mchakato wa amani na mkataba uliosainiwa karibu mwaka mmoja uliopita.

Ni katika mantiki hii ambapo mawaziri hawa wawili watakutana mjini Bamako na Gao wawakilishi wa MINUSMA, Ujumbe wa Umoja wa Ulaya na kikosi cha jeshi la Ufaransa la BARKHANE.

Mapambano dhidi ya ugaidi, maendeleo na masuala ya uhamiaji pia yamo katika katika ajenda ya hatua ya Jumanne nchini Niger.

"Tumekuja pamoja ili kuonyesha dhamira ya Ufaransa na Ujerumani kwa kuunga mkono mchakato ambao unaendelea. Lakini pia ni ujumbe wa Ulaya," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.