Pata taarifa kuu
AMNESTY-UHALIFU-USALAMA

Amnesty International yaonyesha maovu yaliotendwa barani Afrika

Shirika la kimataifa la Amnesty International limewasilisha ripoti yake ya kila mwaka. Ripoti hiyo inaeleza ukiukwaji unaofanywa na makundi ya waasi, lakini pia na serikali katika nchi mbalimbali barani Afrika. Nchi nyingi za Afrika zinanyooshewa kidole kwa ukandamizaji wa wanaharakati wa upinzani na maandamano ya amani.

Kwenye picha hii iliyopigwa Desemba 15, 2015, umati wa watu wakikusanyika karibu na mwili wa mmojwa waandamanaji kutoka jamii ya Oromo katika mji wa Wolenkemi, kilomita sitini kutoka mji wa Addis Ababa, Ethiopia.
Kwenye picha hii iliyopigwa Desemba 15, 2015, umati wa watu wakikusanyika karibu na mwili wa mmojwa waandamanaji kutoka jamii ya Oromo katika mji wa Wolenkemi, kilomita sitini kutoka mji wa Addis Ababa, Ethiopia. AFP
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International inatiwa wasiwasi kuona hatua za kiusalam zinakwenda sambamba na mapambano dhidi ya ugaidi au makundi ya watu wenye silaha. Amnesty International imeitaja nchi ya Cameroon au Niger, ambapo mamia ya watu wanaotuhumiwa kuunga mkono kundi la Boko Haram wanawekwa kizuizini kiholela na kwa muda mrefu.

Amnesty International imezungumzia nchi kadhaa za Afrika zinazoweka usalama kwa kukandamiza upinzani na kutaka waandishi wa habari wasalie kimya.

Shirika hili limeitaja Ethiopia ambapo watu zaidi ya 800 waliuawa tangu kuanza kwa maandamano ya watu kutoka jamii ya Oromo mwezi Novemba 2015. serikali ilirejelea mara kadhaa kwamba inapambana dhidi ya ugaidi, kwa lengo la kuwakandamiza wanasiasa au wafuasi wa vyama vya upinzani

Amnesty imezungumzia matumizi ya nguvu katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, wakati wa maandamano ya upinzani au upande mwingine katika mkoa wa Pool nchini Congo.

Amnesty inatiwa hofu zaidi kuona watu wanaofanya uhalifu huo hawaadhibiwi. Vikosi vya usalama havifunguliwi mashitaka kwa maovu vinavyotenda. Na nchi kadhaa kama vile Burundi, Kenya na Afrika Kusini walichua uamuzi wa kutishia au kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) , baada ya kunyooshewa kidole kwa maovu maafisa wao wa usalama na ulinzi wanayotenda.

Ripoti ya Amnesty Internation imebaini kwamba nchi 23 zimehusishwa katika uhalifu wa kivita mwaka 2016.

Amnesty wamshutumu Trump na viongozi wengine kuhusu wakimbizi

Shirika la Amnesty International limemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wengine nchini Uturuki, Hungary na Ufilipino.
Shirika hilo limesema viongozi hao wanaendeleza kile inachokitaja kuwa kuwatumia vibaya wakimbizi, kwa manufaa yao ya kisiasa, badala ya kutanzua kiini hasa kilichowafanya wakimbizi hao kuyakimbia mataifa yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.