Pata taarifa kuu
AU-ICC-USHIRIKIANO

Umoja wa Afrika kujiondoa katika mahakama ya ICC

Viongozi wa Afrika waliokutana mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, waliunga mkono mpango wa Kenya wa kujiondoa kwa pamoja katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Jengo la kisasa ambalo ni makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa ikiwa ni zawadi ya China kwa Afrika. Ujenzi wa jengo hili uligharimu Dola Milioni 200.
Jengo la kisasa ambalo ni makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa ikiwa ni zawadi ya China kwa Afrika. Ujenzi wa jengo hili uligharimu Dola Milioni 200. CTBUH
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wengi wa mataifa ya Afrika wanahisi kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee.

Viongozi wa Afrika wanasema kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ilifanya makosa kwa kumlenga rais wa Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

"Tathimini yetu ni kwamba ICC inalenga mataifa ya Afrika, hasa viongozi wa nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na viongozi walio madarakani, wakati ambapo kwingineko duniani, mambo mengi yanayotokea, ukiukwaji mkubwa ulio wazi wa haki za binadamu, lakini hakuna kiongozi anayefuatiliwa, "alisema Jumapili rais wa Chad Idriss Deby.

"Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na sheria iko juu kwa kila mtu," alisema Deby, Jumamosi baada ya kuchaguliwa kwa rais mpya wa Umoja wa Afrika. "Kwa hiyo tumeamua kutoa msimamo wetu kwa kusubiri Mahakama ya ICC ichukuwe hatua muhimu kwa msimamo wa viongozi wa Afrika kuhusu suala hili," Bw Deby aliongeza.

Hakuna uamuzi sahihi uliochukuliwa na ykila nchi ina haki ya kuamua iwapo itajiondoa au la katika mahaka ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Lakini serikali ya Kenya ambayo kwa muda mrefu imekua ikikosoa Mahakam ya ICC ilitoa pendekezo kwa Umoja wa Afrika ili kuendeleza mkakati kwa wa nchi za Afrika kujiondoa katika Mahakam ya ICC, "pendekezo ambalo lilipitishwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.