Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Wanasiasa nchini DRC wakubaliana namna ya kumteua Waziri Mkuu

Wanasiasa wa serikali na upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamekubaliana kuhusu sifa za Waziri Mkuu atakayeteuliwa na ukubwa wa Baraza la Mawaziri.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yamekuwa yakiongozwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, baada ya mkataba wa kisiasa kutiwa saini Desemba 31 mwaka 2016.

Christophe Lutundula Apala mmoja wa wajumbe katika mazungumzo hayo ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa, Radio Okapi kuwa wamekubaliana kuwa Waziri Mkuu atakayeteuliwa, atakuwa ni mtu anayetimiza masharti ya kikatiba na kisheria kuhudumu katika nafasi hiyo ya kisiasa.

Imekubaliwa kuwa, Waziri Mkuu atatokea katika upande wa muungano wa vyama vya upinzani vya Rassemblement.

Kuhusu ukubwa wa Baraza la Mawaziri, kutakuwepo na Mawaziri na Manaibu wao 46.

Mazungumzo hayo yanaendelea siku ya Ijumaa, na kikubwa kinachojadiliwa ni ugawanaji wa majukumu katika serikali mpya itakayoundwa ili kutekeleza kikamilifu mkataba wa kisiasa.

Maaskofu nchini humo wameitaka Umoja wa Mataifasa kusaidia kufanikisha utekelezwaji wa mkataba huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.